Press Release (Swahili Version): Uzinduzi wa GenEm Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Press Release (Swahili Version): Uzinduzi wa GenEm Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
share 1

Dodoma, Novemba 4, 2022 Hii ni taarifa kwa vyombo vya habari, Chuo kikukuu cha Dodoma na taasisi ya Empower Limited, tunatangaza ushirikiano rasmi unaoenda kuzindua programu inayoitwa Generation Empower kwakifupi (GenEm). Programu hii inaendana na ajenda ya mabadiliko ya uchumi wa Tanzania kwa kufanya uwekezaji katika kuwapatia vijana wa kitanzania ujuzi. Ushirikiano huu utawezesha taasisi za elimu na sekta binafsi kushirikiana kupitia uratibu mzuri na utekelezaji wa mpango wa kutoa ujuzi unaotakiwa kwa vijana katika karne ya Ishirini na moja.

Ushirikiano huu ni muendelezo wa jitihada tulizoanza mnamo mwaka 2020, tulipoingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na uzinduzi kufanyika na Chansela, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hivi karibuni pia, tumefanya uzinduzi wa programu hii katika Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino Tanzania, jijini Mwanza tarehe 31 Oktoba 2022. Ushirikiano huu utawezesha taasisi za elimu na makampuni kushirikiana kupitia uratibu mzuri na utekelezaji wa mpango wa kutoa ujuzi unaotakiwa katika karne ya Ishirini na moja, katika vyuo vyote nchini.

Empower ni moja kati ya makampuni ya kizawa na kizalendo, inayoelewa changamoto zinazowakumba vijana katika soko la ajira nchini. Kampuni yetu inauzoefu wa zaidi ya miaka 13 katika tasnia ya rasilimali watu nje na ndani ya Tanzania, tukiwaunganisha vijana na fursa mbali mbali zilizopo katika soko la ajira na hivyo tunatambua umuhimu wa kuwawezesha vijana ili wawe na fani na ujuzi sahihi unaohitajika. Empower imejitoa kwa asilimia mia moja kutoa huduma hii kwa wanafunzi wote wa UDOM bila gharama yoyote, ikionesha nia yake ya dhati ya kuwekeza katika taifa letu kwa kujenga jamii yenye vijana welevu na weledi watako kuwa na uwezo wa kutambua na kutatua changamoto zinazolikabili taifa letu na kukuza uchumi wa Tanzania.

Programu hii itasimamiwa na idiara ya vijana kutoka taasisi ya Empower ikishirikiana na uongozi wa chuo. Hadi sasa, taasisi ya Empower ni mdhamini mkuu wa programme hii lakini pia kuna wadhamini mbalimbali kutoka sekta binafsi. Tunao wadau waliodhamini programu kwa muhula huu watatu nayo ni makampuni kama Zulu Lands Engineering Works, Yellow Card, Green Resources na Kilombero Valley Teak Company. Mchango wao unatuwezesha kutanua wigo wa programu kwa kuwafikia vijana wengi zaidi nchini. Tasisi ya Empower inajivunia kuwa waasisi wa programmu hii kwani tunauelewa mzuri kuhusu sekta binafsi na mahitaji ya fani na ujuzi kwa vijana nchini. Asilimia 100 ya wafanyakazi wataasisi ya Empower ni vijana hivyo tunatambua uwezo wa vijana katika kutatua chagamoto za jamii endapo watapewa uwezo na fursa sahihi.

Ushirikiano wetu na Chuo Kikuu cha Dodoma ni wa miaka mitano na tunamalengo ya kuwafikia vijana zaidi ya elfu mbili (2000) kwa UDOM pekee na vijana wengine elfu tano (5000) kutoka maeneo mengine nchini. Vijana watakaofuzu katika programu hii watapata fursa mbalimabali kama kupata ajira kupitia wadau wetu wa sekta bianfsi, fursa za mafunzo ya ujasiriamali, namna ya kutafuta na kupata mitaji ya kuanzisha na kukuza biashara na taarifa muhimu juu ya ujuzi unaohitajika katika fani mbalimabli. GenEm itafanya kazi sambamba na mipango ya kitaaluma ya chuo kuwapa wanafunzi ujuzi bobevu unaotakiwa kwa sasa. Pamoja na kuuwaunganisha katika fursa za ajira pindi watakapohitimu masomo yao, pia makampuni yatanufaika sana na wahitimu hawa wenye ujuzi mkubwa na vipaji ambao wanaweza kuongeza ufanisi katika shughuli zao kutokana na kufanya kazi kwa ubunifu.

Mafunzo ya programu ya GenEm yataendeshwa kwa njia shirikishi na kwa vitendo zaidi, wanafunzi watashiriki katika semina za kubadilishana mawazo kutoka kwa wataalamu na kupata mada kutoka kwa viongozi wa sekta mbalimbali. Hivyo basi Empower pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma tunawakaribisha wadau wote kushiriki katika programu ya GenEm ikiwemo sekta binafsi, watunga sera na mashirika wahisani, ili kufanikisha jitihada za kutoa na kuendeleza ujuzi kupitia mpango wa ubia.

Program hii ni ya kwanza kuanzishwa nchini na kuendeshwa kwa njia ya kipekee ambapo maudhui ya mafunzo yatakayotolewa yata simamiwa na chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania kuhakikisha yanakidhi viwango vinavyotakiwa.

Mwisho Kabisa

Empower is a vibrant, Tanzanian Human Capital Consulting Firm that exists to unite, excite, and nurture people for collective growth. With a global reach and local presence, Empower is the market-leader for recruitment & outsourced services, learning & development, employee engagement, strategic insight and youth impact projects. Our brand is our voice, and our values are our heart. Since 2009, Empower has stayed true to our values. That is the secret to our team success and how we make incredible things happen. Contact youth@empower.co.tz www.empower.co.tz Talent | Advisory | Insight | Youth | Brand.

The University of Dodoma is located about 8 km east of the city centre, and is accessible by public transport, which is easily available from the city centre. Given the central location of Dodoma, UDOM is strategically positioned to serve applicants around the country and specifically government and private sector employees living in Dodoma, who hitherto could not find training opportunities in the area. Such employees can comfortably utilise UDOM to combine work and study for their career advancement. Additionally, the geographical location and Dodoma weather render UDOM a convenient place for international students. 

share 1

Empower Limited
Written by

Empower Limited

Global reach, local presence.

Join #TheMovement Now

Empower helps millions of job seekers and employers find the right fit every day. Start hiring now on Africa’s #1 job site.*

Become a Mover

What People Say About Us