Press Release (Kiswahili Version): GenEm Launch at St. Augustine University of Tanzania Press Release (Kiswahili Version): GenEm Launch at St. Augustine University of Tanzania
share 0

Mwanza, Oktoba 31, 2022 Hii ni taarifa kwa vyombo vya Habari, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino na taasisi ya Empower Limited, tunatangaza ushirikiano rasmi unaoenda kuzindua programu inayoitwa Generation Empower kwakifupi (GenEm). Programu hii inaendana na ajenda ya mabadiliko ya uchumi wa Tanzania kwa kufanya uwekezaji katika kuwapatia vijana wa Kitanzania ujuzi. Ushirikiano huu utawezesha taasisi za elimu na sekta binafsi kushirikiana kupitia uratibu mzuri na utekelezaji wa mpango wa kutoa ujuzi unaotakiwa kwa vijana katika karne ya Ishirini na moja.

Taasisi ya Empower ni kampuni ya kizawa yenye mlengo wa vijana. Uzoefu wetu wa zaidi ya miaka 13 katika tasnia ya rasilimali watu nchini na nje ya Tanzania umetuwezesha kuona umuhimu wa kuwasaidia vijana wa kitanzania na umekutusukuma kuanzisha programu hii yenye lengo la kubadilisha mitazamo ya vijana. Taasisi ya Empower imejitoa kwa asilimia miamoja kutoa huduma hii kwa vijana wote nchini bure kabisa ikionesha nia ya dhati ya kuwekeza katika taifa letu kwa kujenga jamii yenye vijana welevu na weledi watako kuwa na uwezo wa kutambua na kutatua changamoto zinazolikabili taifa letu na kukuza uchumi wa Tanzania.

Programu hii itasimamiwa na idiara ya vijana kutoka taasisi ya Empower ikishirikiana na uongozi wa chuo. Hadi sasa, taasisi ya Empower ni mdhamini mkuu wa programme hii lakini pia kuna wadhamini mbalimbali kutoka sekta binafsi. Tunao wadau waliodhamini programu kwa muhula huu watatu nayo ni makampuni kama Zulu Lands Engineering Works, Yellow Card, Green Resources na Kilombero Valley Teak Company. Mchango wao utatuwezesha kutanua wigo wa programu hii kwa kuwafikia vijana wengi zaidi nchini. Tasisi ya Empower inajivunia kuwa waasisi wa programmu hii kwani tunauelewa mzuri kuhusu sekta binafsi na mahitaji ya fani na ujuzi kwa vijana nchini. Asilimia 100 ya wafanyakazi wataasisi ya Empower ni vijana hivyo tunatambua uwezo wa vijana katika kutatua chagamoto za jamii endapo watapewa uwezo na fursa sahihi.

Program hii ilianza rasmi mwaka Septemba, 2020 na ilizinduliwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mtaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama Chancellor wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mchakato huu ni muendelezo wa jitihada tulizoanzisha tukishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Dira yetu ni kufikia vijana wote nchini kupitia taasisi za elimu hususani elimu ya juu ili kutoa mafunzo haya na kuwasaidia vijana wa kitanzania.

Ushirikiano wetu na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino ni wa miaka mitano na tunamalengo ya kuwafikia vijana zaidi ya elfu mbili kwa SAUT pekee. Vijana watakaofuzu katika programu hii watapata fursa mbalimabali kama kupata ajira kupitia wadau wetu wa sekta bianfsi, fursa za mafunzo ya ujasiriamali, namna ya kutafuta na kupata mitaji ya kuanzisha na kukuza biashara na taarifa muhimu juu ya ujuzi unaohitajika katika fani mbalimabli. GenEm itafanya kazi sambamba na mipango ya kitaaluma ya chuo kuwapa wanafunzi ujuzi bobevu unaotakiwa kwa sasa. Pamoja na kuuwaunganisha katika fursa za ajira pindi watakapohitimu masomo yao, pia makampuni yatafaidika sana na wahitimu hawa wenye ujuzi mkubwa na vipaji ambao wanaweza kusaidia kuongeza ufanisi katika shughuli zao kutokana na kufanya kazi kwa ubunifu.

Akizungumza na waandishi wa habari chuoni Mwanza, Mkuu wa Chuo Amb. Prof. Costa Ricky Mahalu alisema, “Tunachofundisha hapa mara nyingi ni nadharia tu na hata tunapokwenda kwenye practical sehemu fulani fulani bado wanafunzi wanatoka hawajaiva vizuri. Waajiri sasa hivi hawataki ukajifunze kazi ukiwa kazini kwani ni gharama kubwa. Ni vyema kuwa na mfumo wa elimu unaoendana na karne ya sasa inavyowenda.”

Mafunzo ya programu ya GenEm yataendeshwa kwa njia shirikishi na kwa vitendo zaidi, watashiriki katika semina za kubadilishana mawazo kutoka kwa wataalamu na kupata mada kutoka kwa viongozi wa sekta mbalimbali. Hivyo basi Empower pamoja na chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania tunawakaribisha wadau wote kushiriki katika programu ya GenEm ikiwemo sekta binafsi, watunga sera na mashirika wahisani, ili kufanikisha jitihada za kutoa na kuendeleza ujuzi kupitia mpango wa ubia. Program hii. ni ya kwanza kuanzishwa nchini na kuendeshwa kwa njia ya kipekee ambapo maudhui ya mafunzo yatakayotolewa yata simamiwa na chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania kuhakikisha yanakidhi viwango vinavyotakiwa.

Mwisho Kabisa

Empower is a vibrant, Tanzanian Human Capital Consulting Firm that exists to unite, excite, and nurture people for collective growth. With a global reach and local presence, Empower is the market-leader for recruitment & outsourced services, learning & development, employee engagement, strategic insight and youth impact projects. Our brand is our voice, and our values are our heart. Since 2009, Empower has stayed true to our values. That is the secret to our team success and how we make incredible things happen. Contact youth@empower.co.tz www.empower.co.tz Talent | Advisory | Insight | Youth | Brand.

St. Augustine University of Tanzania is a private university in Mwanza, Tanzania. It was founded by the Catholic Bishops of Tanzania in 1998 as a secular, nonprofit, private institution. Before 1998, SAUT was called first Nyegezi Social Training Centre and then Nyegezi Social Training Institute. https://www.saut.ac.tz/ 

share 0

Empower Limited
Written by

Empower Limited

Global reach, local presence.

Join #TheMovement Now

Empower helps millions of job seekers and employers find the right fit every day. Start hiring now on Africa’s #1 job site.*

Become a Mover

What People Say About Us